Jumamosi, 18 Machi 2017

Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya Mbinguni?

Swali: "Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya Mbinguni?"

Jibu: Mimi ni mtu mzuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni. “Sawa, kwahivyo nafanya mambo mabaya, lakini zaidi nafanya mambo mazuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni.” Mungu hatanipeleka Jehanamu kwasababu siishi kulingana na Bibilia. Nyakati zimebadilika!’’ “Watu wabaya pekee kama vile watesaji watoto na wauaji huenda Jehanamu.”

Haya yote ni mafikira ya kawaida kati ya wengi, lakini ukweli ni kwamba yote ni uongo. Shetani mtawala wa dunia, huyapanda mafikira/mawazo haya akilini mwetu. Yeye na yeyote afuataye njia zake ni adui wa Mungu (1Petro 5:8). Shetani hujigeuza na kujifanya mzuri (2Wakorintho 11:14), lakini anauwezo juu ya akili zote ambazo hazimwelekei Mungu. “Shetani, Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake. Hawaielewi injili kuhusu utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu” (2Wakorintho 4:4).

Ni uongo kuamini ya kwamba Mungu hashuhuliki na dhambi ndogo, na kwahivyo Jehanamu imetengewa “Watu wabaya.” Dhambi zote zinatutenganisha na Mungu, hata “ile dhambi ndogo nyeupe.” Wote wamefanya dhambi, na hakuna atoshaye kuwa mzuri wa kujifikisha Mbinguni yeye mwenyewe (Warumi 3:23). Kuingia Mbinguni haitegemei kwamba uzuri wetu uwe unazidi ubaya wetu, Sote tungelishindwa kama hiyo ndiyo hali. Na ikiwa wanaokolewa kwa neema yake Mungu, basi sio kwa matendo yao mazuri. Kwasababu hiyo, neema yake Mungu isingekuwa kama jinsi ilivyo-ya huru na isiyostahili (Warumi 11:6). Hatuwezi kufanya lolote jema lakutuwezesha kufika Mbiguni (Tito 3:5). Unaweza kuingia katika ufalme wa Mungu kwakupitia mlango ulio mwembamba pekee. Njia ya Jehanamu ni pana na mlango wake ni mpana kwa walio wengi wachaguao njia ya rahisi (Mathayo 3:13). Hata kama kila mtu anaishi maisha ya dhambi, na kumwamini Mungu hakumo, Mungu hatasema hivyo. “Ulikuwa ukiishi kama kawaida ya ulimwengu huu, uliojaa dhambi, ukimtii Shetani mfalme wa uwezo wa anga. Yeye ni roho atendaye kazi katika mioyo ya wale wakataao kumtii Mungu” (Waefeso 2:2).

Wakati Mungu alipoumba ulimwengu, ulikuwa kamili. Kila kitu kilikuwa kizuri. Halafu akamuumba Adamu na Hawa na akawapa uhuru ili waweze kuwa na chaguo kama watamfuata na kumtii Mungu au la. Lakini Adamu na Hawa, wanadamu wa kwanza kabisa Mungu alioumba walidanganywa na Shetani wamuasi Mungu, na wakatenda dhambi. Hii iliwatenganisha (na kila aliyekuja baada yao pamoja na sisi) na uwezo wakuwa na uhusiano wakaribu na Mungu. Yeye ni mkamilifu na hawezi kuwa penye dhambi. Kama watu wenye dhambi, hatungeliweza kufika huko sisi wenyewe kwahivyo, Mungu akatengeza njia ili tuweze kupatanishwa naye huko mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Yesu alizaliwa ili aweze kutufundisha / kutuonyesha njia na afe kwa ajili ya dhambi zetu. Siku tatu baada ya kifo chake, alifufuka toka kaburini (Warumi 4:25), akishuhudia ushindi wake juu ya mauti. Aliliunganisha pengo kati ya Mungu na mwanadamu ili tukaweze kuwa na uhusiano wa kibinafsi naye kama tutaamini.

“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana17:3). Watu wengi wamwamini Mungu, hata Shetani pia. Lakini kupokea wokovu, ni sharti tumregelee Mungu, tujenge uhusiano wa kibinafsi, tuziache dhambi zetu na tumfuate yeye. Ni sharti tumwamini Yesu kwa kila kitu tulicho nacho na kwakila tunachofanya. “Tunafanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu tunapomwamini Yesu Kristo atuchukulie dhambi zetu. Na sote tunaweza kuokolewa namna hii, haijalishi sisi ni kina nani au tumefanya nini’” (Warumi3:22). Bibilia inafundisha yakuwa hakuna njia nyengine yoyote ya wokovu isipokuwa kupitia kwa Kristo. Yesu asema katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Yesu ndiye njia ya pekee ya wokovu kwasababu yeye pekee anaweza kutulipia adhabu ya dhambi zetu (Warumi 6:23). Hakuna dini nyengine yoyote ifundishayo kwa kina au uzito wa dhambi na madhara yake. Hakuna dini nyengine yoyote inayogarimia malipo ya dhambi isipokuwa Yesu pekee. Hakuna “mwanzilishi wa dini” mwengine ambapo Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana1:1, 14) - njia ya pekee ya kuweza kulipa deni. Ilibidi Yesu kuwa Mungu ili aweze kutulipia deni. Ilibidi Yesu afanyike kuwa mwanadamu ili aweze kufa. Wokuvu unapatikana kwa imani ndani ya Yesu Kristo! “Wala hakuna wokovu katika mwengine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya Mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili 

Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya Mbinguni?

Tafuta Habari Njema

Maswali muhimu sana Maswali yanayo ulizwa zaidi kila mara

TafutaHabari NjemaMaswali muhimu sanaMaswali yanayo ulizwa zaidi kila mara

Tafuta: 

© Copyright 2002-2017 Got Questions Ministries - All Rights Reserved.
www.gotquestions.org/Kiswahili - Maswali ya Bibilia yajibiwa

Jumatano, 4 Januari 2017

NAMNA YA KUOMBA

NAMNA YA KUOMBA
 – Hatua na vipengele muhimu katika kuomba 


1– MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17 Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya. Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake. Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake. Tii kila Uongozi anaokupa. 


2.FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7 Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako binfsi; (i) – Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata kama hawajaja kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15) (ii) – Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa. Hata kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)


 3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148 Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa. Ndio maana Neno linasema; ‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye atakupa haja za moyo wako’ (Zab37:4). Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.


 4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26 Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza mahitaji yako binafsi; (i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4) Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine. (ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11) Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya. ‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good things and big things) 


 5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5 Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’, kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.


 6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo uliloliombea na kulipata. Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14) 


7. MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu. Ndipo ufunge maombi yako. MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16 -Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa 43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa. -Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa. “Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)

Jumamosi, 31 Desemba 2016

BLESS ISRAEL

shalom...
there are something i wanna share with you or i can say i wanna remainder you...
its about to bless ISRAEL
i say that because of our blessing, the word of god in GENESIS 12:3 its say that "i will bless those who bless you, i will curse him who curses you; and in you all the families of the earth shall be blessed"
those are word of god that GOD was say with Abraham......
i wanna tell you that we needed to pray for israel, we needed to bless israel....
with that we should blessed a lot am telling you...